Urejesho ni mchakato wa kurudisha kitu kilichoharibika au kupotea. Biblia inatuhimiza kumgeukia Mungu. Na kupitia imani na maombi, tutapata uponyaji, kurejeshewa nguvu, na kupewa maisha mapya katika Kristo Yesu.

‭Yer‬emia 30:17‬
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA …
‭‭Yoe‬li ‭2:25‬ ‭
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

Mnamo mwaka 2022, Familia ya Ev. Mchome, ilipitia kipindi kigumu sana baada ya kumpoteza mama yao mpendwa (Aliyeanguka ghafla na kufariki). Majonzi na simanzi kubwa ilitanda mioyoni mwao mithili ya wingu zito na giza totoro, hakuna maneno mazuri ambayo yangetosha kuwapa faraja familia hii.

Video

https://www.youtube.com/watch?v=AwXP9okjjbE&pp=ygUmTmVlbWEgR29zcGVsIENob2lyIE5pa3VyZWplc2hlZSAoTGl2ZSk%3D

Shares:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *