Haya ni maombi mazuri kwa yule anae hitaji kuona mkono wa Bwana.
Ibrahimu alimuita Mungu Bwana anaetenda kwa maana hivyo ndivyo Mungu alivyo jifunua kwake
Musa alimuita Mungu Bwana fahari yangu kwa maana hiyvo ndivyo Mungu alivyo jifunua kwake
Na wewe, ambia Mungu ajifunue kwako ili umpe jina jipya kadiri na atakavyo jifunua kwako.
Lyrics
Mda wako ni huu Bwana
Shuka na nguvu, shuka
Watu wako tunangojea
Shuka na nguvu, Shuka
Tusirudi jinsi tulivyo Kuja
Mkono wako utende tutambue uko hapa
Alama za uwepo wako
Zionekane ijulikane ya kwamba
Eh Bwana uko na sisi
Tenda oh oh oh tenda
Ujifunue hapa Yesu tenda
Sema oh oh oh sema
Utuongoze hapa Yesu sema
Tupe ushuhuda, tukupe jina mpya
Inayo fanana na jinsi umejifunua